Bayern Munich wameungana na Paris St-Germain katika mbio za kumsajili winga wa Chelsea na Morocco Hakim Ziyech, 29. (Fijaches - in Spanish)
Mlinzi wa kati wa RB Leipzig na Croatia Josko Gvardiol, 21, anasema anataka kucheza katika Ligi ya Premia na alikuwa karibu kujiunga na Leeds United mnamo 2020 na karibia angesajiliwa na Chelsea msimu uliopita wa joto. (Times – Subscription Required)
Mmiliki wa Chelsea Todd Boehly hana nia ya kumfuta kazi meneja Graham Potter licha ya kushindwa kwa The Blues 1-0 na Southampton Jumamosi. (Mirror)
Barcelona wanamfuatilia kwa karibu kiungo wa kati wa Manchester City na Uhispania Rodri kabla ya dirisha la majira ya joto na watakuwa tayari kutoa pauni milioni 80 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Football Insider)
Tottenham wanamtaka meneja wao wa zamani Mauricio Pochettino kama mbadala wa Antonio Conte ikiwa Muitaliano huyo ataondoka Spurs mwishoni mwa msimu huu. (Nicolo Schira)
Newcastle United inamfuatilia kwa karibu beki wa Arsenal na Scotland Kieran Tierney, 25. (Football Insider)
Familia ya Glazer imepewa usaidizi wa kifedha wa kusalia kama wamiliki wa Manchester United na Uongozi wa Hedge fund wa Marekani Elliott baada ya kikundi hicho chenye makao yake makuu mjini New York kusajili nia ya kuwekeza katika klabu hiyo. (ESPN)
Inter Milan ndio walio mstari wa mbele kumsajili mshambuliaji wa Borussia Monchengladbach na Ufaransa Marcus Thuram, 25, mbele ya Manchester United na Bayern Munich. (Calciomercato – in Itali )
Chelsea na Tottenham wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Brighton wa Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson, 18. (Sun)
Sevilla wana nia ya kupata mkataba wa mkopo kwa beki wa pembeni wa Manchester City Mhispania Sergio Gomez, 22. (Fijaches - in Spanish)
BBC