Simba katika mtego mwingine dhidi ya Azam Fc

Joel JJ By Joel JJ
β€’
20 Feb 2023
Simba katika mtego mwingine dhidi ya Azam Fc

Kikosi cha Azam Fc kimekuwa kambini kwa takribani wiki mbili kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumanne katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Mchezo huo una umuhimu wa kipekee kwa kila timu ili kufanikisha malengo ya msimu huu

Simba iko kwenye mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu ikiwa nyuma kwa tofauti ya alama sita dhidi ya Yanga

Matokeo ya ushindi yatawafanya wapunguze gap la pointi kuwa tatu kabla ya Yanga haijacheza na KMC siku ya Jumatano

Azam Fc wamepoteza matumaini katika mbio za ubingwa, vita yao kubwa iko katika nafasi ya tatu baina yao na Singida Big Stars

Ushindi kwao utawahakikishia wanarudi kwenye nafasi ya tatu

Afisa Habari wa Azam Fc Thabit Zakaria 'Zakazakazi' amesema wamejipanga kushinda mchezo huo kama walivyofanya katika mchezo wa duru ya kwanza

Simba itaingia katika mchezo huo ikiwa imetoka kujeruhiwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa wakikubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Raja Casablanca

Lakini ni mchezo ambao wanahitaji sana kushinda ili kurejesha morali ya kikosi kabla ya kusafiri nchini Uganda kuikabili Vipers Fc Februari 25

ADVERTISE HERE

More Stories

De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
49m ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
2h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
3h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
4h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
5h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
7h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
9h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
10h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
11h ago
READ MORE β†’