Liverpool na Real Madrid wanakutana kwa mara nyingine kwenye hatua ya mtoano ligi ya mabingwa barani Ulaya huku Liverpool ikiwa na rekodi mbaya dhidi ya mabingwa hao wa kihistoria barani Ulaya
Miezi tisa imepita tangu Liverpool waangukie pua kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa kufuatia kipigo cha 1-0 dhidi ya Mabingwa hao mara 14
Real Madrid itakosa huduma ya wachezaji wake muhimu Mjerumani, Toni Kroos na Mfaransa, Aurelien Tchouameni kwa majeruhi huku Karim Benzema akitarajiwa kurejea baada ya kukosa mchezo uliopita wa Ligi.
Mechi nyingine itawakutanisha miamba ya Ujerumani, Eintracht Frankfurt dhidi ya vinara wa Serie A, Napoli katika dimba la Deutsche Bank Park.