Klabu ya soka ya Geita Gold imezindua rasmi mfumo wa kusajili wanachama kidigitsli
Akizungumza leo katika mkutano na wanahabari Katibu mtendaji wa klabu Saimon Shija amesema kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo ibara ya 5 inawatambua wanachama kama sehemu ya kuiongoza klabu na kufanya maamuzi.
"Licha ya kuwa klabu inamilikiwa na Halmashauri kwa kiwango kikubwa lakini katiba inatoa nafasi kwa wanachama kuwa sehemu ya umiliki"
Mwanachama atajiunga kwa kuchangia shilingi elfu 3 kwa Mwezi sawa na shilingi elfu 36 kwa mwaka na atasajiliwa katika mfumo maalumu wa wanachama kwa utaratibu ulioweka na klabu.
Aidha Mwanachama baada ya kusajiliwa atapokea kadi yake ya uachama iliyo katika mtindo wa kidigitali
"Kwa kuzingatia pia kuwa tunawachama na mashabiki kutoka pande zote za Tanzania tumezindua namba Maalumu ya kuchangia na kulipia ada ya uachama ya LIPA NAMBA 5215290 GEITA GOLD FOOTBALL CLUB
"Klabu imekusudia kupokea wanachama wasiopungua elfu 2 kwa Mwaka kama sehemu ya kuimarisha timu. Aidha mpango huu wa kusajili wanachama ni endelevu na tutafanya jitihada kubwa kuimarisha mfumo huu na kuwa na klabu yenye ukubwa na ushindani lakini pia kuongeza nguvu ya kiuchumi ndani ya klabu"