Tetesi za soka Ulaya, Jumatano Februari 22 2023

Joel JJ By Joel JJ β€’ 22nd February 2023


Tetesi za soka Ulaya, Jumatano Februari 22 2023

Kiungo wa kati wa Chelsea N'Golo Kante, 31, anatazamiwa kusaini mkataba mpya na klabu hiyo huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa akikaribia kurejea kutokana na jeraha. (Telegraph – Subscription Required)

Aston Villa wako tayari kusikiliza ofa kwa mlinda mlango Emiliano Martinez, 30, ambaye aliisaidia Argentina kushinda Kombe la Dunia mwaka jana. (Mail)

Manchester United haitarajiwi kubadilisha uhamisho wa mkopo wa mshambuliaji wa Uholanzi Wout Weghorst mwenye umri wa miaka 30 kutoka Burnley kuwa uhamisho wa kudumu wakati wa dirisha la usajili la majira ya kiangazi. (Football Insider)

Leicester City wanajaribu kumshawishi kiungo mchezeshaji James Maddison kusaini mkataba mpya, lakini watataka kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 msimu wa joto ikiwa haitaonekana kama atasalia katika klabu hiyo.

Manchester City, Newcastle United na Tottenham wanavutiwa na mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza. (Football Insider)

Meneja wa Brighton Roberto de Zerbi, 43, anavutia vilabu vikuu katika nchi yake ya Italia, huku pia akihusishwa na Tottenham. (Telegraph - usajili unahitajika)

Winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha, 30, amekataa ofa nyingi za kuongeza kandarasi yake ya Eagles na klabu ya Al Nassr, ambayo ilimsajili fowadi wa Ureno Cristiano Ronaldo, 38, ni miongoni mwa klabu tatu za Saudi Arabia ambazo zimemtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast. (Evening Standard)

Mtaalamu wa lishe wa Al Nassr Jose Blesa anasema wachezaji wote wanafanya mazoezi kwa bidii na kufuata mpango wa lishe tangu kuwasili kwa Ronaldo. (Ideal, via Mirror)

Arsenal wanatayarisha ofa ya kumnunua mshambuliaji wa Atalanta na Denmark Rasmus Hojlund, 20. (La Repubblica – in Italian)

Mshambulizi wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 24, hajakataa kuondoka katika klabu hiyo ya Italia msimu huu wa joto na anasema kuvutiwa na vilabu vikubwa vya Ulaya kunatoa motisha ya ziada ya kucheza vyema kwa ajili yake na timu yake. (ESPN)

Leeds United wanapanga kumnunua mshambuliaji wa Sweden Viktor Gyokeres, 24, ambaye mkataba wake na Coventry City utaendelea hadi majira ya joto 2024. (Teamtalk).

Kiungo wa kati wa Urusi Arsen Zakharyan, 19, hatahamia Galatasaray kutoka Dynamo Moscow, licha ya timu hiyo ya Uturuki kumtaka. (Fabrizio Romano)

BBC


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.