Liverpool - Real Madrid

Liverpool hoi mbele ya Real Madrid

Joel JJ By Joel JJ
22 Feb 2023
Liverpool hoi mbele ya Real Madrid

Real Madrid ilitokea nyuma na kupata ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Liverpool katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 bora Ligi ya mabingwa barani Ulaya

Wenyeji Liverpool walifunga bao la kwanza kwenye Uwanja wa Anfield Darwin Nunez akimchambua kipa wa Real Madrid Thibaut Courtois 

Wakionekana kuwa katika ubora mkubwa, Liverpool wakaongeza la pili katika dakika ya 14 baada ya Mohamed Salah kutumia makosa ya mlinda lango Courtois

Hata hivyo Real Madrid walirejea mchezoni ambapo Dakika ya 21 Vinicius Junior aliifungia Real Madrid bao la kwanza

Vinicius tena akafanya matokeo kuwa 2-2 katika dakika ya 36 akitumia makosa ya mlinda lango Alisson

Wageni Real Madrid walirejea kipindi cha pili wakiwa wa moto kwelikweli, Mbrazil Eder Militao akaongeza bao la tatu kabla ya Karimu Benzema kuongeza mecngine mawili

Liverpool wamejiweka katika nafasi ngumu ya kutinga robo fainali kwani sasa watahitaji kupata ushindi huko Hispania

Lakini matokeo haya yanaweza yasiwashangaze mashabiki wa Liverpool kutokana na mwenendo wa timu yao msimu huu

Katika mchezo mwingine uliopigwa jana, Eintracht Frankfurt walikubali kipigo cha mabao 2-0 nyumbani dhidi ya timu bora kwa wakati huu barani Ulaya, Napoli

More Stories

BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
1h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
1h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
2h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
3h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
3h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
3h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
3h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
5h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
15h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
15h ago
READ MORE →