Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Februari 23 2023

Joel JJ By Joel JJ β€’ 23rd February 2023


Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Februari 23 2023

Arsenal wako tayari kumenyana na Borussia Dortmund, Newcastle na Juventus kuwania saini ya beki wa kulia wa Real Valladolid raia wa Uhispania Ivan Fresneda, 18. (Standard)

Kipa wa England Jordan Pickford, 28, anakaribia kusaini mkataba mpya na Everton. (Times - subscription required)

Arsenal pia wameanza mazungumzo ya kuongeza mkataba na kiungo wa kati wa Uswizi Granit Xhaka, 30, ambaye ana nia ya kusalia Emirates Stadium. ( 90,min)

Liverpool wanavutiwa na mlinzi wa RB Leipzig na Croatia Josko Gvardiol, 21. (Fabrizio Romano)

Beki wa Ureno Joao Cancelo, 28, anasema uhamisho wake wa mkopo kwenda Bayern Munich ilikuwa fursa ambayo hangeweza kuikataa baada ya kuamini kwamba anafaa kucheza zaidi Manchester City, huku meneja Pep Guardiola akipinga. (O Jogo, via Mail)

Mkurugenzi wa Shakhtar Donetsk Darijo Srna anasema klabu hiyo itajaribu kumsajili tena fowadi wa Ukraine mwenye umri wa miaka 22 Mykhailo Mudryk siku zijazo baada ya kuhamia Chelsea mwezi uliopita. (Football Ramble, via Football.london)

Ajenti wa kiungo wa kati wa Austria Marcel Sabitzer amedokeza kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 anaweza kusalia Manchester United hadi mwisho wa msimu huu kufuatia uhamisho wake wa mkopo kutoka Bayern Munich. (Sport 1 – In Germany )

Rais wa Napoli Aurelio de Laurentiis ameipa Manchester United matumaini ya kumsajili mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 24, baada ya kusema "wakati mwingine kuna ofa ambazo huwezi kukataa". (Mirror)

Leicester City wanaweza kutafuta kumsajili kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na Ujerumani Mahmoud Dahoud, 27, kwa uhamisho wa bila malipo msimu wa joto. (Leicester Mercury)

Kipa wa zamani wa England Ben Foster, 39, anasema hajutii kukataa nafasi ya kustaafu na kusaini Newcastle, ambayo kipa wake chaguo la kwanza Nick Pope amepigwa marufuku kwa fainali ya Kombe la Carabao Jumapili. (TalkSPORT)

BBC


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.