Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira 'Robertinho', amesema wanakwenda Uganda kusaka ushindi dhidi ya Vipers Fc ili kufufua matumaini ya kutinga robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Akizungumza muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kuelekea Uganda, Robertinho amesema wachezaji wake wako tayari kwa mchezo huo na watahakikisha wanashinda ugenini
"Tumejipanga kushinda mchezo dhidi ya Vipers bila kujali tupo ugenini najua haitokuwa rahisi, lakini nikwambie tu ninaimani kubwa na jeshi langu la wachezaji 24 tutafanya maajabu tukiwa ugenini," alisema Robertinho.
Wachezaji 24 waliosafiri jioni ya leo ni Aishi Manula, Beno Kakolanya, Ally Salum, Shomari Kapombe, Izrael Mwenda, Mohamed Hussein, Gadiel Michael, Kennedy Juma, Mohammed Ouattara, Joashi Onyango, Henock Inonga na Erasto Nyoni.
Wengine ni Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin,Clatous Chama, Ismail Sawadogo, Saido Ntibazonkiza, Peter Banda, Kibu Denis, Pape Sakho, John Bocco, Jean Baleke, Moses Phiri na Habibu Kyombo.