Arsenal wamemweka kiungo wa kati wa West Ham na Uingereza Declan Rice, 24, juu ya orodha inayosakwa msimu huu kwani The Gunners hawana uwezekano wa kuwa na fedha za kuwania kumnasa kiungo wa kati wa Borussia Dortmund anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 150 Jude Bellingham, 19. (Football.London)
Hata hivyo, Rice angebadilisha safu ya kati ya Liverpool iwapo atajiunga na Reds, kulingana na kiungo wa zamani wa klabu hiyo Dietmar Hamann. (TalkSport)
Bellingham, wakati huohuo, hajakatishwa tamaa na matokeo mabaya ya hivi majuzi ya Liverpool na anasalia kushabikia klabu hiyo na kocha wa Reds Jurgen Klopp. (Athletic Subscription)
Manchester United wanataka kuimarisha safu yao ya ulinzi kwa kumsajili beki wa kati wa Napoli na Korea Kusini Kim Min-jae, 26, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 42. (Corriere dello Sport – In Itali)
Wakati huo huo, United wana nia ya kumpa mkataba mpya wa muda mrefu fowadi wa Argentina na mchezaji anayechezea wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 Alejandro Garnacho. Mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 unamalizika msimu wa joto wa 2024 na klabu inataka kumzawadia nyongeza kubwa ya mshahara. (Mail)
Kiungo wa kati wa Liverpool na Brazil Fabinho, 29, anaweza kuuzwa baada ya miaka mitano Anfield huku mkufunzi Jurgen Klopp akitafuta kukiburudisha kikosi chake msimu wa joto. (Mirror)
Tottenham wanaongoza katika harakati za kumsajili kiungo wa kati wa Leicester City na Uingereza James Maddison, 26. (Football 365)
Mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 29, hataki kurejea Chelsea baada ya muda wake wa mkopo katika klabu ya Inter Milan kukamilika mwishoni mwa msimu. (90 min)
Everton wanaweza kumnunua fowadi wa Udinese Mreno Beto, 25, msimu wa joto baada ya ofa "kubwa" kwa mchezaji huyo kukataliwa Januari. (Liverpool Echo)
Arsenal iliwasilisha ofa ya euro 70m (£61.7m) kwa Barcelona kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji wa Brazil Raphinha, 26, mwezi Januari. (Sport – In Spanish )
Mshambuliaji wa zamani wa West Ham na Everton Enner Valencia anakaribia kujiunga na klabu ya Brazil Internacional kutoka Fenerbahce, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Ecuador mwenye umri wa miaka 33 akitarajiwa kuhama kwa uhamisho wa bila malipo.(Fabrizio Romano).
Chelsea wanakaribia kufikia makubaliano ya mdomo na Independiente del Valle kumsajili kiungo wa kati wa Ecuador Kendry Paez, 15, ambaye ataweza kujiunga atakapofikisha umri wa miaka 18. (Fabrizio Romano).
BBC