Neymar amepata majeraha ya kifundo cha mguu na huenda akashindwa kuivaa Bayern Munich itakapoikabili Paris Saint-Germain katika mechi ya pili ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alitolewa nje kwa machela wakati PSG iliposhinda mabao 4-3 dhidi ya Lille Jumapili iliyopita.
Baada ya kufunga bao la pili la PSG, Neymar aliumia kifundo cha mguu wake wa kulia katika changamoto na Benjamin Andre mapema kipindi cha pili.
PSG ilithibitisha baadaye Neymar hajaumia lakini sasa imethibitika kuwa aliumia.
Kwa mujibu wa gazeti ma France Football, muda wa kawaida wa kupona jeraha kama hilo ni kati ya wiki sita na nane, hali itakayomfanya akose mechi ya mkondo wa pili itakayochezwa Machi 8, mwaka huu.
PSG, ambao watamenyana na Marseille kwenye Ligue 1 Jumapili, wataelekea Munich wakiwa nyuma kwa bao 1-0.