Simba

Hatujakata tamaa - Phiri

Joel JJ By Joel JJ
β€’
24 Feb 2023
Hatujakata tamaa - Phiri

Mshambuliaji wa Simba, Moses Phiri, amesema licha ya matokeo mabaya ambayo wameyapata mfululizo, lakini wao kama wachezaji bado hawajakata tamaa kwa ajili ya kuipigania timu hiyo kufanya vizuri.

Simba imeshindwa kupata ushindi katika michezo mitatu iliyopita ya michuano yote ambapo imepoteza miwili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya na Raja Casablanca, kisha wakapata sare ya bao 1-1 dhidi ya Azam FC.

Phiri amesema wao kama wachezaji bado hawajakata tamaa na wanaamini hiki ni kipindi cha mpito kwani watarejea katika ubora wao na kupata matokeo mazuri ya kuwapendeza Wanasimba wote

"Kwenye mpira hiyo ipo, lakini najua ni ngumu kwa mashabiki kuvumilia haya kwa kuwa wanaumizwa na matokeo wakiwa wanatamani kufurahi katika kila mchezo"

"Sisi wachezaji tunafahamu na tunawaahidi mashabiki wetu kuwa tutapambana katika michezo ijayo tuweze kupata matokeo mazuri mara baada ya kushindwa kupata matokeo hayo katika michezo mitatu iliyopita, mashabiki watafurahi kwani na sisi hatupendezwi na matokeo haya," alisema Phiri

Phiri ni mmoja wa wachezaji wa Simba waiosafiri Uganda kwa ajili ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Vipers Fc ambao utapigwa Jumamosi, Februari 25

GPL

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
1h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
1h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
1h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
5h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
9h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
10h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
11h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
12h ago
READ MORE β†’