Wananchi wako Mali ambapo Jumapili jioni watashuka Stade du 26 Mars kuikabili Real Bamako katika mchezo wa raundi ya tatu hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika
Kwa mara ya kwanza nyota wawili wa Yanga Mamadou Doumbia na Djigui Diarra wanarejea Mali lakini sasa wakibeba ramani ya ushindi wa Yanga dhidi ya timu ya nyumbani kwao
Doumbia alisajiliwa na Yanga dirisha dogo, lakini bado hajaingia kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Nasreddine Nabi

Ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa na soka la Mali, alikuwa nahodha wa kikosi cha Mali kilichokwenda kushiriki michuano ya CHAN nchini Algeria
Ni wazi Nabi huenda akamtumia katika mchezo huo kama ilivyo kwa Djigui Diarra kutokana na uzoefu wao na soka la Mali
Real Bamako sio wepesi licha ya kupoteza mchezo wa kwanza ugenini kwa kufungwa mabao 3-1 na TP Mazembe na kisha kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya US Monastir nyumbani
Tayari wamedondosha alama mbili nyumbani, wataweka nguvu kubwa zaidi katika mechi mbili zilizobaki nyumbani wakianza na mechi dhidi ya Yanga Jumapili
Alama moja kwa Yanga ugenini hayatakuwa matokeo mabaya lakini alama tatu yatakuwa matokeo bora zaidi ambayo yataiweka Yanga katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali