Simba

Ni Vipers Fc dhidi ya Simba leo

Joel JJ By Joel JJ
25 Feb 2023
Ni Vipers Fc dhidi ya Simba leo

Simba iko nchini Uganda ambapo leo majira ya saa 1 usiku itashuka uwanja wa St Marry's Kitende kuwakabili wenyeji wao Vipers Fc katika mchezo wa raundi ya tatu michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Mechi muhimu sana kwa Simba nchini Uganda, kwani dakika 90 za mchezo huo zitaamua hatma, malengo ya Simba katika michuano hiyo msimu huu

Baada ya kupoteza mechi mbili za kwanza, kimahesabu Simba bado ina alama 12 za kuwania mezani, ushndi utarudisha matumaini ya kusonga ya kwenda hatua ya robo fainali kwani Simba bado itakuwa na mechi mbili nyumbani ambazo kama watashinda watakuwa na uhakika wa kukusanya alama tisa kabla ya mechi ya mwisho dhidi ya Raja ambayo itapigwa Morocco

Lakini matokeo tofauti na ushindi yatafifisha matumaini hayo ya Wekundu wa Msimbazi, watahitaji muujiza kuweza kutinga robo fainali

Hivyo mechi ya leo ni moja kati ya zile mechi kubwa ambazo Simba ilihitaji kucheza kibingwa kuweza kuibuka na ushindi

Simba imekuwa na rekodi nzuri kwenye mechi za ugenini katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu

Walishinda mechi zote za ugenini kwenye raundi za awali dhidi ya Nyasa Big Bullets na Primero De Agosto na kama wachezaji wangekuwa makini, wangepata matokeo mazuri katika mchezo wa kwanza wa makundi dhidi ya Horoya Ac ambao walipoteza kwa bao 1-0

Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira amesema wanatambua mchezo huo utakuwa mgumu sana lakini wako Uganda kusaka ushindi

Kabla ya kutua Simba, Robertinho alikuwa akiinoa Vipers Fc hivyo anawafahamu vyema na leo kazi itakuwa moja tu kwa Simba, KUWAPIGA

More Stories

Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
4h ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
4h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
7h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
7h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
8h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
8h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
8h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
8h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
9h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
10h ago
READ MORE →