Mshambuliaji wa Paris St-Germain na Argentina Lionel Messi anatafakari juu ya uwezekano wa kurejea kwenye klabu yake ya utotoni ya Newell's Old Boys. (UOL, via Mirror)
Mshambuliaji wa Chelsea na Ureno Joao Felix, 23, anataka kuufanya mkataba wake kutoka Atletico Madrid uwe wa kudumu msimu huu. (Fijaches - in Spanish)
Liverpool wanataka kusiani mkataba na kiungo wa kati wa Bayern Munich na Uholanzi Ryan Gravenberch, 20, kucheza sambamba na mchezaji wa England na Borussia Dortmund Jude Bellingham, 19. (Express)
Mmiliki wa Chelsea Todd Boehly anaangalia uwezekano wa kuinunua klabu ya Ligue 1 ya Strasbourg. (L'Equipe)
Liverpool, Newcastle, Tottenham na West Ham ni miongoni mwa klanbu za Primia Ligi are zinazomfuatilia kwa karibu kiungo wa kati wa mainz na Ujerumani Anton Stach, 24. (90min)
Matheus Franca ambaye alikuwa analengwa na Newcastle amesaini mkatababa mpya na Flamengo, ambao walikataa ofa ya Magpies ya pauni £17.5m kwa ajili ya kiungo huyo wa kati Mbrazili mwenye umri wa miaka 18 mwezi Januari. (Sun)
Fulham, Everton, Leicester na West Ham wanamtaka mlinzi wa Roma na England Chris Smalling, 33. (90min)
Newcastle United wanapanga uhamisho kwa ajili ya kiungo wa kati-nyuma wa Wolves Muingereza Max Kilman mwenye umri wa miaka 25. (Football Insider)
LA Galaxy wanamtaka kiungo wa kati wa Chelsea Mbrazil Andrey Santos, 18, baada ya mpango wao wa pendekezo la kumchukua kwa mkopo kuvunjika . (Goal)
Brazil inaweza kumleta meneja wa zamani wa Uhispania na Barcelona, Luis Enrique kuchukua nafasi ya Tite badala ya meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti. (Fijaches - in Spanish)
BBC