Mtanange wa fainali kombe la Carabao kati ya Manchester United dhidi ya Newcastle United unapigwa dimba la Wembley huko Uingereza leo
Hii ni nafasi kwa Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag kuhesabu taji lake la kwanza akiwa na Man United lakini anakutana na Newcastle United yenye roho ngumu kwelikweli
Newcastle tangu wapate mataji wapya, wamekuwa sio timu rahisi kupata ushindi dhidi yake
Mchezo utapigwa saa 1:30 usiku kwa saa za Tanzania




