Yanga yapata alama moja muhimu Mali

Joel JJ By Joel JJ β€’ 26th February 2023


Yanga yapata alama moja muhimu Mali

Yanga imefanikiwa kuondoka na alama moja nchini Mali baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Real Bamako katika mchezo wa raundi ya tatu, kundi D Kombe la Shirikisho barani Afrika

Yanga ilikuwa bora kwa muda mwingi wa mchezo na hakika matokeo haya wachezaji hawawezi kuyafurahia kwa sababu walikaribia kuondoka na alama zote tatu

Fiston Mayele alifunga bao la Yanga kwenye dakika ya 60 baada ya pasi murua kutoka kwa Stephane Aziz Ki

Hata hivyo kukosekana kwa umakini katika kucheza mpira wa kona kuliigharimu Yanga kwenye dakika ya 90 Real Bamako wakisawazisha bao hilo kupitia kwa Emile Kone

Yanga inarejea Dar na alama moja muhimu ambayo imeendelea kuwaweka kwenye nafasi ya pili wakifikisha alama nne nyuma ya US Monastir wenye alama saba

Mapema Monastir waliichapa TP Mazembe mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa DR Congo

Yanga na Real Bamako zitakipiga tena uwanja wa Benjamin Mkapa Machi 08


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.