Kocha Mkuu wa Manchester United Erik Ten Hag leo ameanza kuhesabu taji lake la kwanza akiiongoza United kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Newcastle Unite katika mchezo wa fainali kombe la Carabao uliopigwa uwanja wa Wembley
Mabao mawili ya kipindi cha kwanza kutoka kwa Casemiro na bao la kujifunga Botman yalitosha kuihakikishia Man United ushindi uliowapa taji baada ya miaka sita
Pamoja na kuwa na mechi nzuri kwa muda mwingi, dakika sita zilitosha kuzima ndoto ya Newacatle kushinda taji lao la kwanza tangu mwaka 1969
Ten Hag amefanya mabadiliko makubwa ya uchezaji kwa kikosi cha Man United pengine huu ni mwanzo wa kurejea mataji Old Trafford