Baada ya kurejea kutoka Uganda ambako walifanikiwa kuichapa Vipers Fc bao 1-0 na kufufua matumaini ya kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, kikosi cha Simba kinaanza maandalizi ya mechi mbili zinazofuata katika michuano hiyo ambazo zitapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
March 07 Simba itaikaribisha Vipers Fc katika mchezo utakaopigwa saa 1 usiku kisha kufuatiwa na mchezo dhidi ya Horoya Ac ambao utapigwa March 18
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema wanahitaji kuvuna alama zote sita katika mechi hizo mbili ambazo zitakuwa ngumu
"Asante Mungu Ushindi wetu wa Uganda ni ishara kuwa kazi ya kuitafuta robo fainali inaanza"
"Haitakua rahisi maana Vipers hatakubali kufungwa nje ndani na Horoya hatakubali kupoteza matumaini yake"
"Lakini yote yanawezekana kama kila Mwana Simba atatimiza majukumu yake. Agenda kuu ya Kitaifa ya Wana Simba hivi sasa ni Operation six points eye to the Quarter finals (Mpango ni alama 6 Jicho kwenye Robo Fainali)"
"Kila mwenye silaha, Mwenye mawazo na mwenye mbinu atumie ili azma yetu itimie Kwa mashabiki wenzangu tuanze sasa maandalizi ya March 7, Jukumu letu ni kuujaza Uwanja na kushangilia," aliandika Ahmed kwenye ukurasa wa mtandao wake wa kijamii