Simba

Robertinho ataja mbinu ya ushindi Uganda

King Kong By King Kong
β€’
27 Feb 2023
Robertinho ataja mbinu ya ushindi Uganda

Baada ya kuvuna pointi tatu ugenini dhidi ya Vipers, Kocha Mkuu wa Simba, Robertiho Oliveira, ametambia mfumo mpya kuwasaidia kuibuka na ushindi huku akieleza matokeo hayo yamerudisha uhai mpya katika mipango yao ya kusaka pointi sita za michezo miwili ya nyumbani

Robertinho ameeleza kufurahishwa na kiwango kizuri cha wachezaji katika mchezo wa tatu wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 Uwanja wa St Mary's, Uganda

Bao pekee la Simba lilifungwa na beki Henock Inonga baada ya mpira wa faulo uliopigwa na Mohamed Hussein 'Tshabalala' na kuchezwa kwa kichwa na Sadio Kanoute kisha Moses Phiri kabla ya mfungaji kuuzamisha nyavuni.

Akizungumza jana baada ya kurejea kutoka Uganda, Robertinho alisema kilichomfurahisha ni jinsi walivyocheza kitimu hasa kipindi cha pili huku muunganiko wa wachezaji vijana na wazoefu ukiwa mzuri.

"Wiki yote nilikuwa na kazi ya kubadilisha mfumo wa uchezaji na umeniletea matokeo chanya, nilijua timu yangu ya zamani ina wachezaji wazuri sana, wanacheza mfumo wa 4-3-3 na mimi nimetumia 4-4-2, lakini nimetumia wachezaji vijana kushambulia kama Kibu, Moses Phiri, tumefunga bao moja na kupoteza nafasi mbili ndani ya eneo la hatari, na nimejaribu kuchanganya wachezaji wazoefu na damu changa," alisema kocha huyo

Robertinho alisema jambo jema kwao ni kupata matokeo mazuri katika mchezo muhimu na kurejea nyumbani na pointi tatu bila kujali wameshinda bao ngapi.

"Katika Ligi ya Mabingwa hasa hatua ya makundi ushindi ndio jambo linalotakiwa, iwe moja, mbili au nne kinachoangaliwa ni pointi tatu.

"Tumecheza vizuri, tulikuwa na muunganiko mzuri mbinu yetu ilikuwa kuhakikisha tunapata ushindi kipindi cha pili muunganiko wetu uliimarika, kasi iliongezeka iliyochangiwa na wachezaji vijana na wazoefu," alisema Robertinho.

"Wachezaji wamepambana kwa kucheza kufa kupona katika mchezo ngumu na ushindani mkubwa ambao matokea hayo yametufanya tufufue matumain kuelekea katika michezo miwili inayofuata tukihitaji alama sita"

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
3h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
3h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
4h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
7h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
11h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
11h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
12h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
12h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
13h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
14h ago
READ MORE β†’