Beki wa kulia wa klabu ya PSG na Morocco, Ashraf Hakimi anachunguzwa na Polisi Nchini Ufaransa kwa tuhuma za ubakaji zilizoripotiwa na binti mmoja mwenye umri wa miaka 24 siku ya Jumatatu.
Kwa mujibu wa jarida la Le Parisien, binti huyo ameripoti kufanyiwa kitendo hicho mnamo Februari 24 nyumbani kwa nyota huyo huko Paris lakini hakuwa tayari kufungua mashitaka
Hata hivyo mamlaka nchini humo imelivalia njuga suala hilo na imeanza kufanya uchunguzi wa awali kubaini ukweli juu ya sakata hilo
Klabu ya PSG haijatoa tamko lolote kufuatia sakata hilo. Hakimi ambaye ni mzaliwa wa Uhispania alikuwa sehemu ya kikosi cha Morocco kilichomaliza nafasi ya nne kwenye michuano ya kombe la Dunia la nchini Qatar