Vita ya kuwania kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa katika kundi C ni kubwa hasa kwa klabu za Horoya Ac ya Guinea na Simba ya Tanzania
Baada ya ushindi wa bao 1-0 ambao Simba waliupata dhidi ya Vipers, walifufua matumaini ya nafasi yao wakifikisha alama tatu wakipanda mpaka nafasi ya tatu
Horoya Ac wana alama nne wakiwa wa pili, walipoteza mchezo ugenini dhidi ya Raja Casablanca wakifungwa mabao 2-0
Raja wanaongoza kundi C wakiwa na alama tisa kimahesabu wao wanahitaji alama nyingine tatu tu ili kutinga robo fainali
Mechi za raundi ya nne Simba itakuwa nyumbani dhidi ya Vipers Fc wakati Horoya Ac nao watakuwa nyumbani dhidi ya Raja Casablanca
Tajiri na Mmiliki wa klabu ya Horoya Soufiane Souare ametamka wazi kuwa wana kazi moja tu ya kuhakikisha wanapata ushindi dhidi ya Raja Casablanca kwenye mchezo huo
Soufiane alienda mbali na kusema hata ikiwezekana kwa kutumia mabibi na mababu zake ushindi upatikane!
Miongoni mwa ahadi ambazo amewahidi wachezaji wake ni kuwapa Tsh milioni 100 fedha ambazo watazipata kwa kila bao litakalopatikana dhidi ya Raja Casablanca
Horoya wakifanikiwa kuifunga Raja Casablanca watakuwa katika nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya Robo Fainali



