Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji 'Mo' ambaye ni Rais wa heshima wa klabu, amefanya uteuzi wa Wajumbe wanne wanaoingia kwenye Boci ya Wakurugenzi ya klabu
Walioteuliwa ni Dk. Raphael Chegeni, Mhe Rashid Shangazi, Bwana Hamza Johari na Bwana Zulfikar Chandoo
Katika taarifa aliyotoa mapema leo, Mo amesema uteuzi huo umezingatia uzoefu wao akiwa na imani kuwa watasaidia katika kutimiza lengo la klabu
"Nimeteua wajumbe wanne wapya kwenye Bodi ya Simba Sports Club. Karibu Dk. Raphael Chegeni, Mhe Rashid Shangazi, Bwana Hamza Johari na Bwana Zulfikar Chandoo. Wanachama hawa wataleta uzoefu mkubwa ambao utasaidia katika kutimiza lengo la klabu, na kuwa klabu ya soka inayoongoza barani Afrika"