Manchester United - Crystal Palace

Manchester United, Crystal Palace zapigwa faini

Joel JJ By Joel JJ
β€’
1 Mar 2023
Manchester United, Crystal Palace zapigwa faini

Manchester United na Crystal Palace zimepigwa faini ya pauni 55,000 na chama cha soka nchini England FA kwa kushindwa kuzuia wachezaji wao ambao waliingia kwenye vurugu katika mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa Februari 12, 2023.

Katika mchezo huo kiungo wa United Carlos Casemiro alioneshwa kadi nyekundu baada ya kumkaba shingoni kiungo wa Palace Will Hughes wakati vurugu hizo zikiendelea.

Vurugu hizo zilianza kwa kiungo wa Palace Jeffrey Schlupp kumfanyia madhambi winga wa United Antony na wote wawili wakapewa kadi ya njano.

United wamekubali shtaka hilo huku Palace wakikanusha. Msemaji wa Chama cha Soka alisema:

"Manchester United na Crystal Palace walikubali na kukana kwamba walishindwa kuhakikisha wachezaji wao wanajiendesha kwa utaratibu na kujiepusha na uvunjifu wa sheria na kanuni za soka"

"Tume huru ya udhibiti baadaye ilipata mashtaka dhidi ya Crystal Palace kuthibitishwa na kuzitoza faini za vilabu vyote viwili"

More Stories

Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
3h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
7h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
7h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
8h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
8h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
9h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
10h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
10h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
23h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
1d ago
READ MORE β†’