Baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo, Fc Barcelona, usiku wa kuamkia leo ilirejea katika makali yake baada ya kuwachapa mahasimu wao Real Madrid 1-0 katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Copa del Rey.
Bao la kujifunga la Eder Militao lilizitenganisha timu hizo kwenye Uwanja wa Bernabeu licha ya wenyeji kumiliki mpira na nafasi nyingi.
Ni matokeo muhimu kwa kocha Xavi Hernandez ambaye ametoka kupoteza mechi dhidi ya Manchester United kwenye Ligi ya Europa na Almeria kwenye La Liga.
Kikosi cha Xavi kilijilinda kwa kina baada ya kuongoza na nidhamu yao ilipata faida finyu ya kuingia katika mkondo wa pili Nou Camp mnamo Aprili 5



