Yanga - Geita - Singida BS

Yanga yaifumua Prisons 4-1

Joel JJ By Joel JJ
β€’
3 Mar 2023
Yanga yaifumua Prisons 4-1

Yanga imetinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo ulipigwa uwanja wa Azam Complex

Ulikuwa mchezo uliotawaliwa na Yanga kwa muda mwingi lakini hadi mapumziko hakukuwa na mabao kutoka kila upande licha ya Yanga kufanya majaribio mengi zaidi kwenye lango la Prisons

Hata hivyo Yanga ilirejea ikiwa na kasi zaidi kwenye kipindi cha pili, alikuwa nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto aliyeitanguliza Yanga kwa bao la mapema kwenye kipindi cha pili kabla ya Jumanne Elifadhili hajasawazisha kupitia mpira wa kichwa

Kuingia kwa bao hilo kuiifanya Yanga iongeze kasi ya mashambulizi na kufanikiwa kufunga mabao mengine matatu kupitia kwa Clement Mzize aliyefunga mabao mawili pamoja na Stephane Aziz Ki aliyefunga kupitia mkwaju wa penati

Mzize angeondoka na mpira leo kama angefunga mkwaju wa penati kwenye dakika za majeruhi

Mzize anaongoza mbio za ufungaji bora akiwa amefikisha mabao sita

Mchezo huo ulishuhudiwa na Mwenyekiti wa Makampuni ya GSM, Ghalib Said Mohammed

Aidha klabu ya Singida Bi Stars imetinga robo fainali baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania wakati Geita Gold nao wakitinga robo fainali kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Green Worriors

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
8h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
8h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
9h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
12h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
16h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
16h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
17h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
18h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
18h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
19h ago
READ MORE β†’