Transfer

Tetesi za soka Ulaya, Jumamosi March 04 2023

Joel JJ By Joel JJ
4 Mar 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumamosi March 04 2023

Real Madrid itatathmini mustakabali wa muda mrefu wa Mkroatia Luka Modric, 37, na Mjerumani mwenye umri wa miaka 33 na kiungo mwenza Toni Kroos kabla ya kujitolea kwa kiungo wa kati wa Borussia Dortmund Jude Bellingham, 19, ambaye amepewa ushauri wa kukataa kuhamia Liverpool. (Diario AS - in Spanish)

Real Madrid pia wanamfuatilia kiungo wa kati wa Newcastle Mbrazil Bruno Guimaraes, 25, kwa kipindi kilichosalia cha msimu wa 2022-23 kama chaguo mbadala kwa Bellingham. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Liverpool watakuwa mstari wa mbele katika kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea na Uingereza Mason Mount msimu huu wa joto, ikiwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 hataweza kuafiki mkataba mpya Stamford Bridge. (Mail)

Chelsea wameanzisha tena nia yao ya kumnunua mlinzi wa RB Leipzig Josko Gvardiol, 21, huku Manchester City na Tottenham pia wakimtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Croatia ambaye ana kipengele cha kumuachia cha pauni milioni 97 katika mkataba wake utakaoanza kutekelezwa kuanzia 2024. (Times - subscription required)

Inter Milan wanatumai kumsajili Naby Keita, 28, msimu huu wakati mkataba wa kiungo huyo wa kati wa Guinea utakapomalizika Liverpool na tayari wamefanya mazungumzo ya kutia moyo na wawakilishi wake. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Kiungo wa kati wa Lyon Mfaransa Houssem Aouar, 24, anakaribia kusaini Eintracht Frankfurt kwa uhamisho wa bure baada ya kukataa kuhamia Manchester United. (Sport1)

Barcelona wanaweza kuwauza baadhi ya nyota wao wakubwa huku klabu hiyo yenye matatizo ikitafuta kuongeza pauni milioni 178, na winga wa Brazil Raphinha, 26, akiwa miongoni mwa wale ambao wanaweza kuondolewa. (Sun)

Manchester United wameungana na Chelsea na Arsenal kumfuatilia kiungo wa kati wa Southampton wa Ubelgiji Romeo Lavia, 19. (Mail)

Tottenham wanatazamia kumnunua kiungo wa Bristol City, Alex Scott. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 19 pia anawindwa na Crystal Palace na West Ham. (Sun)

Leicester na Everton wanamfuatilia kiungo wa kati wa Bologna na Scotland Lewis Ferguson, 23. (Nicolo Schira)

Nottingham Forest wanakabiliwa na upinzani mkali wa kutaka kumbakisha kocha Steve Cooper msimu ujao huku vilabu kadhaa vya Premier League vikiwa vimevutiwa na meneja huyo. (Mail)

Mazungumzo yanaendelea kati ya Manchester United na David de Gea. Kipa huyo wa Uhispania, 32, mkataba wake unamalizika msimu wa joto, lakini anatamani kusalia Old Trafford. (Fabrizio Romano)

Manchester United wamepokea maswali juu ya mkopo kutoka kwa vilabu nchini Uturuki kwa ajili ya mshambuliaji wao wa Uingereza Mason Greenwood, 21, ambaye bado amesimamishwa na klabu hiyo licha ya mashtaka ya uhalifu dhidi yake kutupiliwa mbali mwezi Februari. (Telegraph)

Napoli wanasalia na uhakika wa kumbakisha winga wa Georgia Khvicha Kvaratskhelia, 22, licha ya Manchester City, Chelsea, Real Madrid na Barcelona kumwindwa. (90min)

Fulham wanataka kufanya uhamisho wa mkopo wa winga wa Israel Manor Solomon mwenye umri wa miaka 23 kutoka Shakhtar Donetsk kuwa wa kudumu msimu huu. (Standard)

BBC

More Stories

BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
15m ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
30m ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
1h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
1h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
1h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
1h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
2h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
4h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
14h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
14h ago
READ MORE →