Transfer

Tetesi za soka Ulaya Jumapili, March 05 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
5 Mar 2023
Tetesi za soka Ulaya Jumapili, March 05 2023

Barcelona bado wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Ureno Bernardo Silva na Manchester City watakuwa tayari kumruhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ambaye mkataba wake unaisha Juni 2025, kuondoka kwa euro 65m (£57.5m). (Sport -in Spanish)

Man City watatafuta kumleta mlinzi wa Croatia Josko Gvardiol, 21, kutoka RB Leipzig ikiwa watamuuza mlinzi wa Hispania Aymeric Laporte, 28, ambaye anaIvutia klabu ya Paris St-Germain. (Star)

Kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 27, ametambuliwa na Man City kuwa mbadala wa mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani Ilkay Gundogan, 32, ambaye amekuwa akihusishwa na Barcelona. Wachezaji wote wawili mkataba wao unamalizika msimu wa joto. (Football Transfers)

Tottenham wanataka angalau pauni milioni 100 ikiwa watamuuza mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 29, ambaye amebakiza miezi 15 katika mkataba wake wa Spurs, msimu huu wa joto. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong anasakwa na Manchester United lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 hataki kuondoka Barcelona. (Guardian)

Kiungo wa kati wa Ecuador Moises Caicedo huenda akatia saini mkataba mpya na Brighton lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 bado anatarajiwa kuwaniwa na vilabu vikubwa zaidi vya Premier League msimu huu. (Telegraph)

Chelsea wanataka kumsajili mshambuliaji wa Ureno Joao Felix, 23, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Blues kutoka Atletico Madrid, na kiungo wa kati wa West Ham ya Uingereza Declan Rice, 24, msimu wa joto na wanapanga kuwauza wachezaji watano ili kusaidia kufidia gharama hiyo. (Fichajes - in Spanish)

AC Milan inamtaka kiungo wa kati wa Chelsea Ruben Loftus-Cheek na italazimika kulipa euro 25m (£22.1m) ili kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Calciomercato - in Italian)

Kiungo wa kati wa Ivory Coast Franck Kessie amekuwa akihusishwa na kutaka kuondoka Barcelona lakini klabu hiyo ya Hispania haina nia ya kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 msimu wa joto. (Sport - in Spanish)

Mshambuliaji wa Brazil Roberto Firmino hakuwa amezungumza na klabu nyingine yoyote kabla ya kuamua kuondoka Liverpool wakati mkataba wake utakapokamilika msimu wa joto, kwa mujibu wa wakala wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31. (Football Insider)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
7h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
7h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
8h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
11h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
14h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
15h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
16h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
16h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
17h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
18h ago
READ MORE β†’