Arsenal - Manchester City - Liverpool - Manchester United

Arsenal wakomaa kileleni EPL

Joel JJ By Joel JJ
β€’
5 Mar 2023
Arsenal wakomaa kileleni EPL

Arsenal wanaonyesha dhamira yao ya kuutaka ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Bournemouth hapo jana

Ilikuwa mechi ngumu kwa Arsenal ambao walikuwa nyuma kwa mabao 2-0 kabla ya kusawazisha na kufunga bao la ushindi kwenye dakika za jioniii

Reis Nelson ndiye aliyekuwa shujaa wa Arsenal akifunga bao la ushindi kwenye dakika ya mwisho ya nyongeza (97')

Mapema Manchester City ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Newcastle United na kupunguza tofauti ya alama baina yake ya Arsenal kuwa mbili

Lakini ushindi wa Arsenal umerufisha gap hilo kuwa alama tano huku kila timu ikiwa imeshuka dimbani mara 26

Arsenal ina alama 63 wakati Manchester City ina alama 58, vita hii itaamuliwa katika mechi 12 zilizobaki

Leo saa 1:30 usiku Liverpool itakuwa nyumbani kuumana na Manchester United katika mchezo ambao kama Liverpool watashinda basi watafufua matumaini ya kuwania nafasi nne za juu

Baada ya Spurs kuchapwa 1-0 na Wolves, wamesalia na alama 45 wakiwa wamecheza mechi 26

Liverpool wana alama 39 wakiwa wamecheza mechi 24

More Stories

Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
1h ago
READ MORE β†’
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
11h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
12h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
12h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
16h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
19h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
20h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
20h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
21h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
21h ago
READ MORE β†’