Ushindi wampunguzia presha Potter

Joel JJ By Joel JJ β€’ 5th March 2023


Ushindi wampunguzia presha Potter

Welsey Fofana jana alifunga bao pekee la Chelsea walipoibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Leeds na kumpunguzia presha kocha wa timu hiyo Graham Potter

Ulikuwa ushindi wa pili katika mechi 15 zilizopita, ilikuwa lazima kwa Chelsea kupata ushindi kumpunguzia presha kocha wao Potter licha ya mwenyewe kusisitiza kabla ya mchezo kuwa  anaungwa mkono na wamiliki wa klabu

Chelsea wanasalia katika nafasi ya 10 licha ya ushindi huo huku Leeds wakiwa nafasi ya 17 na pointi moja juu ya eneo la kushushwa daraja.

Pamoja na ushindi huo bado mashabiki wa Chelsea hawaonyeshi kuwa na imani na Potter

Usajili mkubwa uliofanywa hauendani na matokeo ambayo Chelsea wameyapata kabla ya ushindi dhidi ya Leeds

Hata hivyo ushindi huo unaweza kuwaongezea morali kupambana katika mechi zilizosalia


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.