Transfer

Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu March 06 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
6 Mar 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu March 06 2023

Manchester United inamfuatilia mshambuliaji wa Roma Tammy Abraham, lakini klabu yake ya zamani Chelsea imekataa kwanza kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, 25, baada ya kujadiliana kuhusu kipengele cha kumnunua tena cha euro 80m (£70.8m) walipomuuza Serie A. . (Athletic - subscription required)

West Ham wako pointi moja juu ya eneo la kushushwa daraja la Ligi ya Premia lakini The Hammers hawana nia ya kumfukuza meneja David Moyes kwa vile wanamuunga mkono Mskoti huyo ili kuboresha matokeo. (Mail)

Newcastle United wana uhakika wa kukubaliana mkataba mpya ambao utamweka kiungo wa kati wa Brazil Bruno Guimaraes, 25, katika klabu hiyo kwa muda mrefu. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Leicester City na Uingereza James Maddison, 26, yuko kwenye orodha fupi ya wachezaji wanaolengwa na Newcastle United majira ya joto, pamoja na kiungo wa kati wa Manchester United na Scotland Scott McTominay. (Football Insider)

Mshambulizi wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, 24, anasema "ana furaha sana" katika klabu hiyo na mustakabali wake hauhusiani na maendeleo ya mabingwa hao wa Ufaransa katika Ligi ya Mabingwa. (Dakika 90)

Mkataba wa mshambuliaji wa Arsenal Reiss Nelson utaisha msimu wa joto na, wakati mazungumzo ya kurefusha mkataba wa Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 23 yanatazamiwa kuendelea, makubaliano hayajakamilika. (90min)

Uhamisho wa mkopo wa mlinzi wa Arsenal Pablo Mari kwenda Monza ulijumuisha ada ya uhamisho ya £5.9m kwa Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 29 ikiwa klabu hiyo ya Italia itaepuka kushushwa daraja kutoka Serie A na kwa sasa wako mbioni kufanya hivyo. (Football London)

Klabu ya Oxford United iko tayari kuwasilisha ombi kwa Charlton Athletic kumnunua meneja Dean Holden baada ya kuachana na Karl Robinson. Mail)

BBC

More Stories

Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
3h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
7h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
7h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
8h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
9h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
9h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
10h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
10h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
1d ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
1d ago
READ MORE β†’