Mshambuliaji wa Liverpool raia wa Misri Mohammed Salah ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi katika Ligi Kuu ya Uingereza katika klabu ya Liverpool baada ya kufikisha mabao 129
Rekodi hii ilikuwa inashikiliwa na Robbie Fowler kwa muda mrefu akifunga mabao 127
Kabla ya mchezo dhidi ya Manchester United hapo jana ambapo Liverpool iliibuka na ushindi wa mabao 7-0, Salah alikuwa na magoli 127,baada ya kufunga magoli mawili amefikisha magoli 129
Salah amekuwa na mwenendo mzuri wa kupachika mabao akitwaa tuzo ya ufungaji bora ligi ya Uingereza mara tatu
Msimu huu Salah amefunga mabao 19 katika michuano yote, mabao 11 kwenye ligi kuu na mabao nane kwenye michuano ya ligi ya mabingwa



