Mwili wa aliyekuwa mchezaji wa timu ya Mtibwa Iddy Mfaume Mobby umesafirishwa leo kuelekea Ngokolo mjini Shinyanga kwa ajili ya mazishi
Beki huyo alifariki jana katika Hospitali ya Benjamini Mkapa mkoani Dodoma wakati akipatiwa matibabu
Daktari bingwa wa magonjwa ya mifupa na majeraha, kutoka Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dk. Alfred Amede amesema walimpokea mchezaji huyo juzi saa 9 usiku akitokea Turiani mkoani Morogoro.
Amesema baada ya kumpokea walimfanyia vipimo na kumlaza na ilipofika jana saa 9 alasiri alifariki dunia
Mobby wakati wa uhai wake alizichezea timu mbalimbali za soka ikiwemo Ruvu Shooting, Geita Gold, Polisi Tanzania zote za ligi kuu
Katika nyakati tofauti pia alikuwa miongoni mwa mabeki wanaounda kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, 'Taifa Stars'



