Arteta aota ubingwa Arsenal

Joel JJ By Joel JJ • 6th March 2023


Arteta aota ubingwa Arsenal

Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta alisifu bao la ushindi la Reiss Nelson katika dakika ya 97 dhidi ya Bournemouth  kwenye Uwanja wa Emirates akiamini ushindi wa mabao 3-2 waliopata unapaswa kuwapa Arsenal imani zaidi ya kuweza kushinda taji la Ligi Kuu England

Arsenal walikuwa nyuma kwa mabao 2-0 Bournemouth wakifunga kupitia kwa Philip Billing na Marcos Senesi

Hata hivyo, Thomas Partey aliifungia Arsenal kwenye dakika ya 62 kabla ya Ben White kusawazisha dakika nane baadaye

Katika dakika za majeruhi, Nelson alipiga shuti kali kutoka nje kidogo ya 18 na kuipatia timu yake ushindi muhimu uliorejesha tofauti ya poniti dhidi ya wapinzani wao Manchester City kuwa tano

"Labda ni wakati wa furaha zaidi ambao tumekuwa nao," alisema Arteta, ambaye aliteuliwa kuwa kocha wa Arsenal Desemba 2019.

"Safari ambayo tumekuwa pamoja na jinsi mashabiki na wachezaji wanavyojituma, nadhani tuko katika nyakati bora sana"

Tangu kufungwa na Man City Februari 15, mwaka huu, Arsenal imeifunga Aston Villa, Leicester City, Everton na Bournemouth.

"Kushinda mechi nne kwenye Ligi Kuu ni ngumu sana na tumecheza mechi tatu ndani ya wiki, ambayo ni ngumu zaidi"

"Nafikiri pamoja na changamoto ambazo tunaweza kupitia, tunapaswa kuwa na imani zaidi tunaweza kutimiza malengo yetu msimu huu," aliongeza Arteta


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.