Baada ya mapitio 'review' ya shauri la mchezaji Feisal Salum 'Fei Toto' dhidi ya Yanga kugonga mwamba TFF,Β leo Machi 6 nyota huyo ametinga ofisi hizo akiwa na barua ya kuomba kuvunja mkataba wake na Yanga.
Fei Toto ametinga TFF na Mwakilishi wake, Jasmine Razack ambaye alizungumza na waandishi wa habari na kueleza nia ya mchezaji huyo
"Ninaomba tuvute subira, leo Feisal kaleta ombi lake naimani kama litashughulikiwa na TFF, chombo pekee kinachoweza kuvunja mkataba wa mchezaji ni TFF," alisema Jasmine
Fei Toto amekuwa kwenye mvutano na klabu ya Yanga kwa takribani miezi mitatu sasa baada ya jaribio lake la kuvunja mkataba na klabu hiyo kugonga mwamba mara mbili
Mchezaji huyo kupitia Wawakilishi wake, ameweka wazi kuwa hataki tena kuitumikia Yanga hivyo hayuko tayari kurejea kunako klabu hiyo licha ya TFF kupitia Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kuthibitisha kuwa Mkataba wake na Yanga ni halali