Mshambuliaji wa PSG Neymar anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa majeraha aliyopata hivi karibuni na hivyo hatakuwa sehemu ya kikosi cha PSG katika mechi zilizobaki msimu huu
Neymar alipata jeraha la kifundo cha mguu (ankle) katika ushindi wa 4-3 wa PSG dhidi ya Lille ambapo alifunga bao moja na atafanyiwa upasuaji Doha, Qatar siku chache zijazo
PSG wametangaza kuwa nyota huyo anatazamiwa kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu ambao utamkosa katika kipindi kilichosalia cha msimu wa 2022/23.
Neymar, 31, hajacheza tangu alipopata jeraha la kifundo cha mguu wakati PSG ilipomenyana na Lille mwezi Februari
PSG wamesema atakuwa nje kwa miezi mitatu hadi minne kabla ya kuanza tena mazoezi ya timu