Simba kumalizana na Vipers Fc leo

Joel JJ By Joel JJ β€’ 7th March 2023


Simba kumalizana na Vipers Fc leo

Michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika leo inaingia raundi ya nne kwa mechi kadhaa kupigwa

Nchini Tanzania klabu ya Simba itakuwa uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Vipers Fc katika mchezo wa kundi C utakaopigwa saa 1 usiku

Baada ya ushindi wa bao 1-0 waliopata kule Uganda, Simba wanahitaji kushinda tena leo ili kuweka hai matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali

Vipers Fc inayoburuza mkia kundi C ikiwa na alama moja, kimahesabu pia inaweza kuwa na nafasi kama itashinda siku ya leo

Ni mechi inayotarajiwa kuwa na ushindani mkali ikitarajiwa kushuhudiwa na mashabiki wengi wa Simba

Mechi nyingine zinazopigwa leo, Al Hilal watakuwa nyumbani kuikabili Cotton Sport (1600H), CR Beluizdad vs El Merreikh (2200H), Zamalek vs Esperance (2200H) na Horoya vs Raja (2200H)


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.