Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya kumuuza mshambuliaji wake kinara wa mabao kwenye ligi kuu ya Wanawake ambaye ni nahodha wa Simba Queens, Opa Clement kwenda klabu ya Besiktas ya Uturuki
Taarifa iliyotolewa na Simba imeeleza kuwa tayari mshambuliaji huyo ameshaondoka nchini kuelekea Uturuki kwenda kuanza maisha mapya ya soka katika timu yake ya Besiktas
Hadi sasa kwenye Ligi ya Wanawake (Serengeti Lite Women's Premier League) mzunguko wa kwanza umemalizika Opa akiwa ndiye kinara wa ufungaji akiwa amepachika wavuni mabao tisa