Michuano ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa inaendelea leo, Benfica na Chelsea walitinga robo fainali jana na leo Bayern Munich watamenyana na PSG na Tottenham watawakaribisha AC Milan
Wiki hii imekuwa nzuri kwa Kylian Mbappe, ambaye alivunja rekodi ya mabao PSG kwa bao lake la 201 katika klabu hiyo siku ya Jumamosi
Ni mafanikio makubwa kwa fowadi huyo mwenye umri wa miaka 24Β lakini sasa leo anapaswa kuibeba PSG katika mchezo dhidi ya Bayern Munich wakiwa tayari wako nyuma kwa bao 1-0 wakipoteza mchezo wa kwanza nyumbani
Mbappe ameshinda mataji yote ya ndani akiwa na PSG isipokuwa Ligi ya Mabingwa
PSG leo watamkosa Neymar ambaye msimu kwa upande wake umemalizika baada ya kupata majeraha ambayo atafanyiwa upasuaji utakaomuweka nje ya uwanja kwa miezi mitatu au zaidi
Ni wazi Mbappe sambamba na Lionel Messi watahitaji kucheza nafasi kubwa zaidi. Lakini ikiwa PSG itatoka kwenye mashindano katika hatua hii ya mapema, itafungua wimbi la uvumi kuhusu hatma ya Mbappe huko Paris
Tottenham hawajashinda mchezo wowote wa mtoano wa Uropa katika mashindano yoyote ya UEFA tangu watinga fainali ya Ligi ya Mabingwa mnamo 2019
Hilo sio jambo pekee ambalo Spurs inakabiliana nalo inapojiandaa kuwakaribisha AC Milan Jumatano usiku.
Imepita muongo mmoja tangu Antonio Conte afuzu kwa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa akiwa kama meneja, na kufuzu hatua ya 16 bora na hatua ya makundi katika kila moja ya kampeni zake nne za mwisho kwenye michuano ya Ulaya
Yawezekana hawatapata nafasi nzuri zaidi ya kufika robo-fainali ya Ligi ya Mabingwa kuliko mwaka huu wanapokutana na timu iliyo katika hali sawa na wao
Wakiwa nyuma kwa bao 1-0, Conte na Spurs wanahitaji kutinga robo fainali mwaka huu kuonyesha timu hii imeimarika kutoka msimu uliopita