Bayern, AC Milan zatinga robo fainali UEFA

Joel JJ By Joel JJ β€’ 9th March 2023


Bayern, AC Milan zatinga robo fainali UEFA

Bayern Munich imeichapa PSG mabao 2-0 katika mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, na kutinga robo fainali kwa jumla ya mabao 3-0.

Wafaransa walipata nafasi nzuri ya kusawazisha bao katika kipindi cha kwanza huku Yann Sommer akipoteza mpira kwenye eneo la hatari, lakini Matthijs de Ligt alikuwa imara kwenye mstari wa goli kumzuia Vitinha kufunga.

Eric Maxim Choupo-Moting aliongeza faida ya wenyeji mara mbili katika dakika ya 61.

Ilikuwa ni makosa ya kiungo Marco Verratti katika eneo la hatari ndiyo yaliyomtengenezea Moting nafasi hiyo, na Bayern ilihakikisha inawaadhibu wapinzani wao.

Serge Gnabry alifunga bao la pili kwenye dakika ya 89, akimalizia shambulizi la kushtukiza

Bayern wanatinga hatua ya nane bora kwa msimu wa nne mfululizo, huku PSG wakitolewa katika hatua hii kwa mwaka wa pili mfululizo

Nao AC Milan wametinga robo fainali baada ya matokeo ya suluhu ya bila kufungana dhidi ya Tottenham Hotspurs

AC Milan walishinda bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Italia


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.