Nyota wa Real Madrid Eden Hazard ana nia ya kusalia na klabu hiyo hadi mwisho wa mkataba wake Juni 2024, imefahamika.
Kabla ya kufanya maamuzi juu ya hatma yake, Hazard alishauriana na watu wake wa karibu huko Madrid mnamo Februari na kufikia maamuzi kuwa amalize mkataba wake
Hazard mwenye umri wa miaka 32 amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara. Tayari ametangaza kustaafu kuitumikia timu ya Taifa ya Ubelgiji
Real Madrid ililazimika 'kuvunja benki' kumng'oa kunako klabu ya Chelsea Madrid ikikubali kulipa Chelsea €100million
Dili hilo lilijumuisha nyongeza zaidi zenye thamani ya hadi euro milioni 160 ingawa sio nyongeza zote zilizolipwa kwa mujibu wa makubaliano lakini gharama yake mpaka sasa imevuka ada ya €101m ambayo Real Madrid ilitumia kumsajili Gareth Bale na hivyo kumfanya Hazard kuwa mchezaji ghali zaidi katika historia ya Real Madrid