Vipers Fc yamtimua kocha

Joel JJ By Joel JJ β€’ 9th March 2023


Vipers Fc yamtimua kocha

Baada ya kuchapwa na Simba katika mechi zote mbili za ligi ya mabingwa, klabu ya Vipers Fc leo imetangaza kumtimua Kocha wake Mkuu Beto Bianchi

Vipers Fc imefikia uamuzi wa kumfuta kazi Beto kutokana na mwendelezo wa matokeo mabaya tangu kocha huyo alipotangazwa kuchukua nafasi ya Robert Oliveira ambaye alijiunga na Simba.

Beto alitangazwa Januari 10, 2023 na katika majukumu yake amekiongoza kikosi cha Vipers kwenye jumla ya mechi saba (7) za mashindano tofauti.

Katika mechi saba (7) alizoiongoza Vipers Fc,  timu hiyo haijashinda mchezo wowote wala kufunga goli ndani ya dakika 90


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.