Tanzania - Taifa Stars - Yanga - Simba

Kocha Stars atizame Ligi za chini pia

Joel JJ By Joel JJ
10 Mar 2023
Kocha Stars atizame Ligi za chini pia

Baada ya wiki iliyopita Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumtangaza Adel Amrouche kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’, beki wa zamani wa Simba na Sigara, Hamis Kondo amemshauri kocha huyo kuwapa nafasi katika timu ya Taifa wachezaji wanaofanya vizuri ligi za chini

Tangu kutimuliwa kwa Kim Poulsen, Agosti 29, mwaka jana, Stars ilikuwa chini ya kocha wa muda Mzambia, Hanour Janza ambaye naye aliamua kurudi kwao baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Klabu ya Zesco United.

Amrouche raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Algeria, ana uzoefu mkubwa na soka la Afrika baada ya kufundisha klabu na timu za taifa katika ukanda wa Kusini, Mashariki Kati na Kaskazini.

Kocha huyo amewahi kuwa kocha bora wa Afrika Mashariki mwaka 2013 wakati akiinoa na kuipa Kenya 'Harambee Stars' ubingwa wa Cecafa Challenge na kabla ya hapo alifika nusu fainali mara mbili akiwa na kikosi cha Burundi.

Kondo ambaye amewahi pia kuichezea CDA alisema Taifa Stars ni ya wachezaji wote ila sifa ni lazima wawe na uwezo mkubwa bila kuangalia anacheza daraja gani.

"Simba na Yanga lazima azipe kipaumbele katika uteuzi wa timu kwa sababu wachezaji wake wana kiwango bora na wanapata uzoefu wa mashindano ya kimataifa ambayo wanashiriki, lakini lazima awaangalie na wachezaji wa chini kama kwenye Championship wapo baadhi wanaweza"

"Ukiwaweka na wale wanakuwa wanajifunza na baadaye watazidi kuwa wazuri na itakuwa ni hazina kwa Taifa," alisema Kondo

Mwanaspoti

More Stories

Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
37m ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
1h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
3h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
3h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
4h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
4h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
5h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
5h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
5h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
7h ago
READ MORE →