Ruvu Shooting imefufua matumaini katika mapambano ya kubaki ligi kuu leo wakipata ushindi muhimu wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City katika mchezo uliopigwa uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya
Valentine Mashaka na Abdulrahman Mussa walifunga mabao ya Ruvu Shooting wakati bao pekee la Mbeya City lilifungwa na Sixtus Sabilo kupitia mkwaju wa penati
Ruvu Shooting wamesogea hadi nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 20, alama moja zaidi ya Polisi Tanzania ambao wana mechi ya kiporo
