KMC

KMC yatoa mapumziko kwa wachezaji

Joel JJ By Joel JJ
10 Mar 2023
KMC yatoa mapumziko kwa wachezaji

Uongozi wa Timu ya KMC FC umetoa mapumziko ya siku 10 kwa wachezaji wake ambapo watapaswa kurejea kambini Machi 19 ili kujiandaa na michezo iliyobakia ya Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania Bara ambapo Aprili 17 itakipiga dhidi ya Geita Gold katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.

Mapumziko hayo yamekuja kutokana na kwamba KMC FC haitakuwa na mchezo kwa mwezi Machi hadi Aprili 17 na hivyo kutoa nafasi kwa wachezaji wake kujipa muda wakujipanga vema kwenye michezo mitano iliyobakia kabla ya kumalizika kwa msimu wa 2022/2023.

Aidha Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni chini ya kocha Mkuu Thierry Hitimana imecheza mchezo wake wa 25 jana dhidi ya Kagera Sugar na kuibuka na ushindi wa magoli mawili kwa sifuri ambayo yalifungwa na Daruweshi Saliboko na hivyo kuvuna alama zote tatu muhimu na kupanda kwa nafasi moja juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.

"Tumewapa wachezaji wetu mapumziko ya siku 10 ili waende wakajiandae vema kumaliza msimu, tulipita kwenye kipindi kigumu ambacho hatukuwa na matokeo rafiki na hivyo jana kupata ushindi ambao umetupa morali ya kujipanga upya tutakaporejea"

"Ukiangalia Ligi ni ngumu na Timu zote zilizopo hivi sasa kila mmoja anataka kupata matokeo jambo ambalo ni zuri hivyo kama Timu ya Manispaa ya Kinondoni tutarudi tukiwa na nguvu, ari na morali nzuri na kumaliza msimu tukiwa kwenye nafasi nzuri"

KMC FC itakaporejea mbali na kukutana na Geita Gold Aprili 17 , pia itakuwa na kibarua kingine dhidi ya Dodoma Jiji, Singida Bigi stars, Tanzania Prisons pamoja na Mbeya City ambapo kati ya hizo mbili zitachezwa nyumbani huku tatu zikipigwa ugenini

More Stories

SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
1m ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
1h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
11h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
12h ago
READ MORE →
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
12h ago
READ MORE →
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
16h ago
READ MORE →
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
19h ago
READ MORE →
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
20h ago
READ MORE →
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
20h ago
READ MORE →
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
21h ago
READ MORE →