Bournemouth yaiduwaza Liverpool

Joel JJ By Joel JJ β€’ 11th March 2023


Bournemouth yaiduwaza Liverpool

Bournemouth wamejiondoa kwenye eneo la kushuka daraja baada ya kuichapa Liverpool bao 1-0 katika mchezo wa Premia uliopigwa leo

Billing alifunga bao pekee la Bournemouth katika mchezo ambao Mohammed Salah alikosa mkwaju wa penati kwa upande wa Liverpool

Ni kipigo kisichotarajiwa kwa Liverpool ambao wametoka kuifumua Manchester United mabao 7-0 katika mchezo wa ligi uliopita

Bournemouth wamefikisha alama 24 na kupanda mpaka nafasi ya 17 wakati Liverpool wamesalia nafasi ya tano wakiwa na alama 42


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.