Simba yataja viingilio mechi dhidi ya Horoya Ac

Joel JJ By Joel JJ β€’ 13th March 2023


Simba yataja viingilio mechi dhidi ya Horoya Ac

Klabu ya Simba imetangaza viingilio vya mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Horoya Ac ambao utapigwa Jumamosi, March 18 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari, Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema wanahitaji mashabiki wengi wajitokeze dimba la Benjamin Mkapa hivyo hakuna mabadiliko katika viingilio vya mchezo uliopita dhidi ya Vipers Fc

"Mechi hii dhidi ya Horoya Ac tunataka kujaza uwanja wa Benjamin Mkapa, hivyo viingilio ni vilevile, Mzunguuko ni Tsh 3,000/-, VIP C ni Tsh 10,000/-, VIP B ni Tsh 20,000/- na VIP A ni Tsh 30,000/-"

"Pia tutakuwa na tiketi za Executive ambazo gharama yake ni kuanzia Tsh 20,000/- kwa ajili ya makampuni na hata watu binafsi yakiwemo matawi ya Simba. Kwa wale watakaokata tiketi hizi watapatiwa kibaki cha kuingia uwanja wa Mkapa na magari yao"

"Tiketi za Platinum pia zitapatikana kwa Tsh 150,000/- zikiwa na huduma maalum pamoja na kifurushi cha Simba"

"Wapinzani wetu Horoya AC watawasili nchini usiku wa kuamkia Ijumaa, March 17 hivyo kwa wale wanaopenda kwenye kuwapokea taarifa hii iwafikie"

Aidha amesema wameandaa hamasa kubwa katika mji wa Dar es salaam ili kuhakikisha wanaujaza uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumamosi

"Tangu kuanza kwa michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu hatujaweza kujaza uwanja, lakini kwenye mchezo dhidi ya Horoya AC tunataka kujaza uwanja wa Benjamin Mkapa. Hawa Horoya pamoja na ukubwa wao, tukiwapigia kelele hawatatoka salama," alisema Ahmed


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.