Shirika la Utangazaji Uingereza (BBC) limemuomba radhi na kumrejesha mtangazaji wa kipindi cha 'Match Of The Day' Gary Lineker na kutangaza ukaguzi huru katika mwongozo wa mitandao ya kijamii
Awali BBC ilimsimamisha kazi Lineker kufuatia posti yake kwenye mtandao wa Twitter akiikosoa Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uingereza juu ya mpango wa Wizara hiyo juu ya Wahamiaji.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Suella Braverman, alifichua mipango ya Serikali ya kuwazuia wahamiaji na wakimbizi ambapo Lineker alifananisha lugha iliyotumika kuweka mipango hiyo na "ile iliyotumiwa na Ujerumani miaka ya 1930".
Katika taarifa yake kufuatia BBC kuomba radhi, Lineker alisema anafurahi tumepata njia ya kusonga mbele na anatazamia kurudi hewani



