Pogba majanga Juventus

Joel JJ By Joel JJ β€’ 14th March 2023


Pogba majanga Juventus

Kiungo wa Juventus, Paul Pogba anatarajiwa kuwa nje kwa angalau wiki tatu baada ya kuumia

Pogba (29) atakosa nafasi ya kujumishwa kwenye kikosi cha Ufaransa kwa ajili ya kuwania kufuzu kwa Euro 2024.

Pogba hakujumuishwa kwenye kikosi cha Juventus kilichocheza na Freiburg wiki iliyopita, pia alikosa mechi ya ushindi wa 4-2 dhidi ya Sampdoria Jumapili

"Leo asubuhi Pogba alikuwa akipiga faulo akahisi maumivu katika paja lake," kocha wa Juve Massimiliano Allegri alisema baada ya mechi ya Jumapili

Taarifa ya klabu ilisema kuwa Pogba alifanyiwa vipimo vya afya siku ya Jumatatu na kwamba amepata majeraha kidogo kwenye paja lake la mguu wa kulia

"Tayari ameanza mchakato wa matibabu ili kuhakikisha anarejea haraka katika majukumu yake," aliongeza Allegri

Juventus wana mchezo wa marudiano dhidi ya Freiburg siku ya Alhamisi, huku Pogba akikosa mchezo wa kwanza baada ya kuchelewa kuungana na timu Jumatano iliyopita

Pogba amecheza mechi mbili pekee akitokea benchi tangu ajiunge tena na Juve kutoka Manchester United msimu uliopita wa joto, huku mechi ya kwanza akicheza Februari 28.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.