Yanga

Kuitwa kwa Fei Toto Stars gumzo

Joel JJ By Joel JJ
14 Mar 2023
Kuitwa kwa Fei Toto Stars gumzo

Kiungo mshambuliaji Feisal Salum 'Fei Toto', ni miongoni mwa wachezaji 31 walioitwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa ajili ya kujiandaa na mechi mbili dhidi ya Uganda za kusaka nafasi ya kufuzu fainali za AFCON 2024 zitakazofanyika Januari hadi Februari mwakani

Fei Toto, ameitwa kwenye timu ya taifa akiwa hayupo kwenye kikosi cha Yanga kinachocheza Ligi Kuu na michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, na hivi karibuni akiwa amewasilisha barua kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), kuomba kuvunja mkataba na klabu yake hiyo.

Awali, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF ilitangaza kuwa Fei Toto ni mchezaji halali wa Yanga, baada ya kutokea mgogoro wa kimkataba baina ya pande zote, ulioanza mwishoni mwa mwaka jana.

Mbali na mchezaji huyo, ambaye hajaonekana uwanjani kwa muda mrefu sasa, taarifa iliyotolewa jana na Idara ya Habari na Mawasiliano ya TFF chini ya Cliford Ndimbo, iliwataja wachezaji waliochaguliwa kujiunga na kikosi hicho ni Aishi Manula, Beno Kakolanya, Mzamiru Yassin kutoka Simba, Metacha Mnata, Kibwana Shomari, Fei Toto, Dickson Job, Bakari Mwanyeto, Mudathir Yahaya na Ibrahi Baka kutoka Yanga.

Wengine ni Datius Peter, David Luhende, Anuary Jabir na Abdallah Mfuko kutoka Kagera Sugar, Yahaya Mbegu kutoka Ihefu, Yasuph Kagoma wa Singida Big Stars, Sospeter Bajana na Abdul Suleiman 'Sopu' wa Azam FC, Edmund John wa Geita Gold, na Khalid Habibu wa KMKM.

Wachezaji wa Kitanzania walioitwa wanaosakata soka la kulipwa nje ya nchi ni pamoja na nahodha Mbwana Samatta kutoka KRC Genk ya Ubelgiji, pamoja Kelvin John ambaye anaichezea klabu hiyo, Simon Msuva wa Al-Qadsiah ya Saudi Arabia, Ramadhani Makame wa Bodrumspor ya Uturuki, Novetus Dismas wa Zulte Waregem ya Ubelgiji, Alphonce Mabula wa FK Spartak Subotica ya Serbia, Ben Starkie anayeichezea Basford United FC ya Uingereza, Haji Mnoga wa Aldershot Town ya Uingereza, Ally Msengi wa Swallows ya Afrika Kusini, Himid Mao wa Ghazi El Mahala SC ya Misri na Said Khamis wa Al-Fujairah ya Falme za Kiarabu.

Kikosi hicho kitakuwa chini ya Kocha Mkuu Adel Amrouche raia wa Algeria aliyetangazwa hivi karibuni, na kupewa jukumu la kukinoa kikosi cha Taifa Stars.

IPP Media

More Stories

SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
1m ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
1h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
11h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
12h ago
READ MORE →
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
12h ago
READ MORE →
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
16h ago
READ MORE →
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
19h ago
READ MORE →
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
20h ago
READ MORE →
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
20h ago
READ MORE →
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
21h ago
READ MORE →