Mikiki mikiki ya kusaka nafasi ya kutinga robo fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya inaendelea leo kwa mechi mbili kupigwa
Manchester City ambao walilazimishwa sare ya bao 1-1 katikc mchezo wa kwanza dhidi ya RB Leipzig uliopigwa Ujerumani, leo wanahitaji kushinda nyumbani ili kutinga robo fainali
Kwa Kocha Pep Guardiola, michuano hii ina umuhimu mkubwa kwake kwani ndio michuano pekee ambayo hajaweza kushinda tangu atue Manchester City
Guardiola ana rekodi mbaya na ligi ya mabingwa kwani tangu alipotwaa taji hilo akiwa na Fc Barcelona mara mbili, hajawahi kushinda tena
Mechi nyingine ni kati ya Porto dhidi ya Inter Milan ambapo wenyeji Porto watahitaji kupindua matokeo ya kuchapwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Italia
Kesho Napoli itachuana na Entracht Frankfurt, wababe hao wa Italia wakiwa mbele kwa mabao 2-0 na mcheo mwingine ni kati ya Real Madrid dhidi ya Liverpool
Madrid wako mbele kwa ushindi wa mabao 5-2 ugenini, wanahitaji matokeo yoyote isipokuwa kufungwa zaidi ya tofauti ya mabao matatu ili waweze kufuzu robo fainali



